Wednesday, March 4, 2009

Shule za Udereva Zimetuangusha?

Tukiwa tunajiuliza maswali mengi kutokana na ongezeko la ajali nchini, na kutafuta suluhisho au sababu za ongezeko hilo, nadhani tuna wajibu wa kujiuliza kama shule za udereva zinatekeleza wajibu wake kwa kutoa mafunzo muafaka au na zenyewe zimetuangusha kwa kuzalisha madereva walio chini ya kiwango? Je, ni nani anafanya tathmini ya mitaala ya shule hizi ili kujua kama inakidhi au inafikia kiwango?Wadau mjadala upo wazi?

1 comment:

  1. Hivi hizi shule kwanza zinasimamiwa na nani? na hadi kuandikishwa nini kigezo? Utakuta kwenye gari watu watu kama 4 au 5 hivi hao wote ni wanafunzi, yaani wanafundishwa bora liende ili mradi mtu ajue kuwasha gari na kulipeleka barabarani. Wiki mbili mtu amefuzu na yuko barabarani anaendesha chombo cha usafiri. Wengine ndio hujifunza juu ya wenzao na leseni ndio za kupeana mradi utoe kitu kidogo sasa wadhani hapo tutafika? wadhani ajali zitapungua kwa staili hii? Wanaohusika waliangalie hili kwa undani.

    ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker