Sunday, March 22, 2009

kUTOKA MOI LEO

Kutoka Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ajali(MOI) Taarifa zinaonyesha kwamba Majeruhi kadhaa wamepokelewa katika Taasisi hiyo wakiwa ni wa ajali mbalimbali zilizotokea sehemu mbalimbali za jiji. Rashid abdulrahim Rashid(24) mkazi wa Ilala alipokelewa MOI saa 7 usiku baada ya kupata ajali ya pikipiki, amepata michubuko na amevunjika mguu sehemu ya paja(femur). Mwingine ni Christina Mlwale(26) ambaye amevunjika mfupa wa karibu na bega(clavicle) na mumewe Magnus Kisinga (32) wote ni wakazi wa Mbezi Louis, walipata ajali ya kugongwa na gari wakiwa katika katika pikipiki walipokuwa njiani kutoka Mbezi kuelekea Kimara. Christina amelazwa katika wodi ya Mwaisela na mumewe alitibiwa na kuruhusiwa. Wengine ni Slavatory Mathias Temba(18) mkazi wa Magomeni,alipata ajali na kuumia kichwa:Paulo Siyanga(51)naye alifikishwa MOI akiwa amevunjika Mguu sehemu ya paja(femur);Mzee Nasser(60) naye alipata ajali na kupata michubuko mwili mzima na kuumia kichwa na wa mwisho ni Ketra Bernard Frank(22) ambaye alipata ajali na kufikishwa MOI akiwa amevunjika mguu.Bwana Jumaa Almasi Afisa Uhusiano wa MOI amethibitisha kuwapokea majeruhi na kwamba wanaendelea vizuri.No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker