Friday, March 27, 2009

Inasikitisha.......Lakini ni Ujasiri Uliyookoa Maisha ya Kichanga!

Ni katika ajali ya basi la Morning Star iliyoua watu wanane.
Katika taarifa ya tarehe 20 machi 2009, nilitoa taarifa ya ajali ya Morning Star iliyoua watu saba, na wengine kadhaa kujeruhiwa. Gari lililopata ajali lina namba za usajili T674 ADY lililokuwa likifanya safari kutoka Dar es salaam kwenda Mloka Rufiji.
Mmoja kati ya abiria waliopoteza maisha ni Bi. Havijawa Omari mkazi wa Tegeta ambaye alikuwa anaenda Kilimani Rufiji katika msiba. kwa mujibu wa ushuda uliopatikana ni kwamba, kabla ya ajali dereva alijaribu sana kuli-'control' gari lakini akashindwa na hatimaye aliwaambia abiria wake kwamba japo anajitahidi anaelekea kushindwa, hibvyo kila abiria amuombe mungu awasaidie watoke salam. Baada ya kusema hivyo, kila mmoja ndani ya basi alikuwa anafikiria ni jinsi gani ya kujiokoa na gari lilizidi kwenda mrama.
Ndipo mama huyu Havijawa Omari, akiwa na mtoto wake mchanga ikamjia akili ya haraka haraka kabla gari halijapinduka, akamtupa mtoto wake mchanga wa miezi 8 nje ya dirisha kwa lengo la kumuokoa. Baada ya kufanya hivyo gari likapinduka na Havijawa akapoteza maisha!
Mtoto wa Havijawa, Tariq Majaliwa, ni mtoto wa kiume wa miezi 8 ambaye sasa hivi analelewa na bibi yake, alivunjika mkono na kupata michuko sehemu ya usoni.
Ni tukio la kusikitisha, lakini Bi. Havijawa alifanya kile ambacho hakikutarajiwa na wengi.Tariq amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya mifupa na Ajali Muhimbili (MOI). Afisa Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi alithibitisha kumpokea mtoto huyo na akasema kwamba anaendelea vizuri.
POLE: Bi Havijawa Mungu ailaze roho yake peponi, mtoto Tariq namwombea Ahueni ya haraka.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker