Thursday, March 5, 2009

MIKANDA NI MUHIMU KWENYE MABASI!


Yafuatayo ni maoni ya Bered Ntabaliba(ntba2006@yahoo.com) yenye kichwa kisemacho "Mikanda ni muhimu kwenye mabasi",kama ilivyoonekana katika gazeti la Mwanachi la 5/3/2009.

Mhariri,
Nimesoma kwa furaha kubwa taarifa kwenye gazeti lako kwamba mabasi ya abiria yatatakiwa kuwa na mikanda itakayovaliwa na abiria wote.Nimesafiri kwa mabasi Mbeya, Dar es salaam, Morogoro, na kwingineko, mabasi mengi hayana mikanda ya abiria, ajali ikitokea watu wanaangukiana na kujigongagonga mpaka kufa.
Naamini kabisa kwamba kwamba kama abiria hao wangekuwa wamefunga mikanda hiyo vifo vingi vingeweza kuepukika kabisa. Askari wa usalama barabarani wanapoingia kukagua mabasi wanachouliza ni mwendo na siyo kuangalia mikanda.

Namwomba Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema afuatilie kwa kina suala hili ili kuokoa maisha ya watu kwa kuhakikisha kwamba abiria wanavaa mikanda wawapo safarini.

2 comments:

  1. Kwa kweli mabasi mengi ya mikani hayana mikanda kabisa na utakuta dereva anaendesha kana kwamba yuko kwenye mashindano ya magari hawazi kuwa amebeba roho za watu. Njiani wanataka kuovertake malori yaani unasafiri roho iko mkononi. Ikifungwa break ya haraka kaka utajikuta umejigonga kwenye kiti cha mbele. Kungekuwa na utaratibu pia wa kuangalia muda aliotoka dereva na muda anaopaswa kufika kama ni safari ya masaa 3 au sita na iwe hivyo. Na abiria tunapaswa kuwa wakali juu ya hili maana maisha yetu ndiyo yanawekwa hatarini.

    ReplyDelete
  2. Hellen, Tatizo baadhi ya abiria wanashangilia magari yanapoenda kwa kasi sana kama hivyo. Ni lazima tuseme No! kwa hizi ajali zisizo za lazima.

    ReplyDelete

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker