Sunday, March 1, 2009

Alama Mpya za Barabarani!



Udereva makini ni pamoja na kuzingatia alama mbalimbali barabarani, pichani ni alama mpya za barabarani ambazo zinaonyesha makundi maalum ya watu wenye ulemavu mbalimbali. Picha hii ilichukuliwa katika Maonyesho ya Wiki ya Usalama Barabarani Kitafaifa yaliyofanyika mkoani Morogoro mwaka jana. Utafiti wa haraka haraka unaonyesha kwamba madereva wengi waliohojiwa hawazijui alama hizi mpya. Kwa maana hiyo ni dhahiri kwamba wanaweza kusababisha ajali kwa kuwa wataendesha bila kuzingatia alama hizo. Je nini kifanyike kuhakikisha kwamba madereva wanazielewa? Maoni ya wadau yanakaribishwa. (Ili kuziona alama hizo vizuri, bofya katika picha ili kuikuza)

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker