Wednesday, March 11, 2009

Tanzania kutumia Mfumo Mpya Kudhibiti Ajali.

Tanzania inakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutumia teknolojia mpya ya elektroniki katika kudhibiti ajali za brabrani.
Teknolojia hiyo pia itasaidia kupunguz uharibifu wa miundo mbinu ya barabara na kubaini magari yaliyozidisha uzito pamoja na kuweka kumbukumbu zake kwenye mfumo wa kompyuta,ikiwemo namba za usajili.
Kampuni ya ushauri wa kihandisi na biashara ijulikanayo kama AfriDeut Consult Ltd ndiyo inayoratibu pamoja na kusimamia mradi wa kuleta teknolojia hiyo nchini chini ya ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU).
Mkurugenzi Mtendaji wa AfriDeut, Godwin Msechu alisema kuwa teknolojia hiyo ambayo inaweza kumpa taarifa dereva ajisalimishe pindi anapofanya makosa, tayari imejaribiwa kwa baadhi ya nchi za ulaya na imeonyesha mafanikio.
"Hii ni teknolojia ambayo siyo ya gharama kubwa lakini itamwezesha mtumiaji wa barabara kupata taarifa za mapema kuhusu usalama wa abiria, watembea kwa miguu na vile vile itamwezeshaa kulinda rasilimali ya barabara", alisema Msechu.
Alisema teknolojia hiyo inatokana na utafiti uliofanywa chini ya mradi ulioendeshwa na nchi takriban 10 za ulaya, chini ya ufadhili wa EU katika kupata mfumo wa juu wa kusimamia usalama wa miundo mbinu ya barabara pamoja nawatumiaji wake.
Alitaja nchi hizo kuwa ni Finland, Sweden, Ujerumani, Hungary, Ufaransa, Uingereza, Austria na Ubelgiji ambazo baada ya kuukamilisha, Tanzania imechaguliwa kuwa nchi ya mfano kwa Bara la Afrika wakati kwa Asia, ilichaguliwa India.
Katika kuelimisha juu ya teknolojia hiyo, Msechu alisema kuwa wataalam wa nchi hizo watatoa elimu ya teknolojia hiyo katika mkutano wa siku mbili utakaofanyika Arusha, machi 19 na 20, mwaka huu.
Alielezea juu ya Tanzania kuingia kwenye teknolojia hiyo, Ofisa Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania, Ephraem Mrema alisema kuwa wanangojea kwa hamu wataalamu hao wafike wajieleze ili wayatathmini.
HOJA:Ngoja tuone kama huu ndio muarobaini wa kuzuia ajali na vifo visivyo vya lazima vinavyotokea kila kukicha

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker