Saturday, March 7, 2009

LEO KUTOKA TAASISI YA TIBA YA MAGONJWA YA MIFUPA NA AJALI MUHIMBILI(MOI)
Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa MOI Bw. Jumaa Almasi wamepokea majeruhi wa ajali mbalimbali kama ifuatavyo; Sunday Mohamed(23) amepokelewa hospitalini hapo akiwa amevunjika mguu baada ya kugongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki. Ajali ilitokea maeneo ya Salasala, Kunduchi.

"Huu ni mfululizo wa ajali ambazo zimeonekana kushamiri zikiwahusisha waendesha pikipiki, kila wiki tunapokea mwendesha pikipiki akiwa amegongwa au kuanguka mwenyewe au amejeruhiwa katika jaribio la kumpora pikipiki". Amesema Bw. Almasi.

Amesema pia wamempokea kijana ambaye amegongwa na gari na kuumia kichwa(Head Injury) na bado hajapata fahamu kuweza kujitambulisha.
Wakati huo huo Kijana Faki Makame(23) aliyeripotiwa kupokewa juzi katika Taasisi hiyo akiwa amepooza mwili mzima baada ya kuvunjika shingo na mgongo,leo ameweza kuongea na kuelezea mkasa mzima ulivyokuwa. Anasema kwamba,walikuwa katika gari la mkaa wakielekea Rufiji. Gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi sana na hicho ndio chanzo cha ajali. Anasema walipofika kijiji cha Mkwandala kabla ya Nyambonde kuna kona mbili kali sana, ya kwanza dereva alifanikiwa kuipita kwa mwendo huo huo lakini kona ya pili alishindwa na gari ikaingia katika shimo na kupinduka. Akasema watu 6 walijeruhiwa, wawili hawakuumia kabisa na yeye ndio ameumia vibaya sana, amepooza kuanzia shingo mpaka miguuni. Pichani ni Faki akiwa amevaa kifaa cha kumsaidia asilisumbue shingo(Neck collar) na picha nyingine inaonyesha akiwa analishwa.

Kwa kweli inasikitisha, kijana ambaye alikuwa anafanya shughuli zake mwenyewe na anajitegemea, sasa amekuwa tegemezi kwa kila kitu. hii yote ni kwa ajili ya uzembe wa dereva!

Usiku huu imetokea ajali mbaya karibu na stendi ya mabasi ya kwenda mikoani baada ya gari moja kusimama katika kivuko cha watembea kwa miguu ghafla na kusababisha gari ya abiria aina ya coaster kusimama ghafla pia, na kusababisha abiria mmoja kutupwa nje ya dirisha la mbele ya gari.Habari kamili nitawaletea kesho.

3 comments:

  1. Hawa waendesha pikipiki jamani sijui hata kuwe na utaratibu gani maana nafikiri tutawapoteza wengi au wengi wao watapoteza viungo. Si hapa tu hata mji wa jirani Morogoro waendesha pikipiki wako rough sana maana kule pikipiki ndio bajaj zao sasa wanagongwa sana na wengi hupoteza maisha. Kuna ward maalum ya majeruhi na wengi ni waendesha pikipiki. Nafikiri watu wa usalama barabarani waangalie la kufanya zaidi juu ya hili maana sasa takwimu zinapanda badala ya kushuka

    ReplyDelete
  2. Hellen nakubaliana na wewe, hali kwa kweli si shwari. Leo nilikuwa naongea na mdau mmoja akanipa taarifa za wapanda pikipiki wa Morogoro na maafa yanayowakuta. Amesema kwamba, sio ajali tu wanauawa na kupigwa sana katika jitihada za kuwanyang'anya hizo pikipiki. Nafikiri wazee wa fedha waaamke kidogo!

    ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker