Monday, March 2, 2009

Mwanafunzi Aanguka Kwenye Gari, Afariki!

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Tuangoma Wilayani Temeke, jijini Dar es salaam, Juma Abdallah(15), amefariki papo hapo baada ya kuanguka kutoka katika gari alilokuwa amepanda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Emanuel Kandihabi(pichani) alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8.00 mchana, katika barabara ya Changarawe iendayo shule ya Sekondari Tuangoma.
Kandihabi alisema gari hilo lenye namba za usajili T735 AGD aina ya KB Pickup lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambuliwa kwa jina moja la Karota, aliyekuwa akielekea Kongowe kutoka Tuangoma ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo.Alisema juhudi za kumtafuta dereva huyo zinaendelea na maiti ya mwanafunzi huyo imehifadhiwa katika hospitali ya Temeke (Habari na Fatma Aziz, gazeti la Mwananchi)

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker