Wananchi wenye hasira wakishirikiana na waendesha pikipiki za kukodi(bodaboda), Wilayani Korogwe, wamewaua kwa kuwachoma moto watu wawili wanaotuhumiwa kuiba kuiba pikipiki ya kijana mmoja aliyelazwa katika hospitali ya Magunga.
Kamnda wa polisi mkoani Tanga, Nyakoro Sirro, alithibitisha habari kuhusu tukio hilo.
Hata hivyo diwani wa Potwe, Rashid Mdachi alidai kuwa limetokana na 'uzembe' wa polisi wilayani Muheza, kushindwa kwenda kuwakamata wahalifu hao mahali walipokuwa wamejificha, katika kijiji cha Kilometa Saba, wilayani Muheza.
Akisimulia tukio hilo, Diwani wa Potwe, Rashid Mdachi, alisema Machi 14 mwaka huu, vijana hao waliouawa, walikwenda Manundu Korogwe na kukodi pikipiki ya Haji Ramadhani na kumtaka awapeleke kijiji cha Bombani kupitia njia ya Potwe, ambako kuna msitu na walipofika katika ya vijiji vya Potwe na kimbo vijana hao walimshusha na kuanza kumkata mapanga kichwani na mikononi hadi alipozirai. Baada ya kuona 'wameshammaliza' wakachukua pikipiki na kupotea. Lakini kijana huyo alijikokota hadi kijiji cha jirani na kupata msaada ndipo watuhumiwa wakaanza kutafutwa na kukamatwa.
Watuhumiwa waliochomwa baada ya kupigwa katika eneo la Manundu wilayani Korogwe ni, Hatibu Tobi(24) Mkazi wa Mnyuzi Korogwe na Juma Denis Kiango(31).
No comments:
Post a Comment