Katika kile kinachoonekana kuwa mashambulizi dhidi ya madereva wa pikipiki, leo mwendesha pikipiki mwingine, Juma Gema(23) amefikishwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) akiwa mahututi baada ya kupata kipiga kizito toka kwa watu wasiofahamika na hatimaye wakatokomea na pikipiki.
Akisimulia mkasa huo nduguwa karibu ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kwamba Juma hufanya kazi ya kubeba abiria na kituo chake ni Soko Jipya mjini Bagamoyo. Anasema jana usiku Juma alipata abiria lakini baada ya kuondoka hawakumuona tena kurudi na ndipo walipoanzisha msako kujua yuko wapi.Jitihada zao hazikuzaa matunda mpaka walipopata taarifa kwamba ameonekana akiwa ametupwa katika mashamba ya mpunga eneo la Bong'wa karibu na njia ya kwenda Dar es salaam.
Alisema pikipiki iliyoibwa nia aina ya SANLAG ambayo thamani yake ni kama shilingi milioni 1.2.
Afisa uhusiano wa MOI, Bwana Jumaa Almasi amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo na akaongeza kwamba bado hajapata fahamu vizuri na madaktari wamesema inaonekana amepigwa kichwani na hivyo kupata maumivu ya kichwa na kupoteza fahamu.
Jana katika blog hii kulikuwa na taarifa ya mwendesha pikipiki aliyeuawa maeneo ya suka jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment