Thursday, March 26, 2009

Ajali Dar......ni ya Daladala!


Moshi Lusonzo wa gazeti la Alasiri anaripoti kwamba ".......Daladala mbili jijini Dar es salaam zimevaana uso kwa uso na kusababisha abiria wake 18 kujeruhiwa na baadhi yao kulazwa hospitalini.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke Emmanuel Kandihabi amesema ajali hiyo ilitokea jana mishale ya saa 3.30 usiku katika barabara ya temeke, pale kwenye Hospitali ya Wilaya ya Temeke.

Akisimulia tukio hilo, kamanda kandihabi ameyataja magari yaliyopata ajali kuwa ni Nissan Civilian lenye namba za usajili T 405 ADZ lililokuwa likitokea tandika kwenda buguruni likiendeshwa na Jamal Juma 30, mkazi wa mkuranga na Toyota DCM lenye namba za usajili T150 AMC lililokuwa likitokea Temeke kwenda Mbagala.

Amesema katika ajali hiyo, watu 18 walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Temeke, ambapo watu 15 kati yao, walitibiwa na kuruhusiwa na watatu wamelazwa hospitalini hapo.

Kamanda Kandihabi amesema dereva wa DCM alikimbia baada ya kutokea kwa tukio hilo na polisi wanaendelea kumtafuta".

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker