Saturday, March 28, 2009

Chenge agonga na kuua!Habari iliyotawala vyombo vya habari leo ni kuhusu ajali iliyomhusisha Mh. Andrew Chenge Mbunge wa Bariadi Mashariki. Habari zilizopatikana ni kwamba ajali ilitokea majira ya saa 10 alfajiri jana katika eneo la Masaki Shule ambapo yeye akiendesha gari lenye namba za usajili T512 ACE aliigonga Bajaj yenye namba za usajili T 736 AXC na kuua watu wawili ambao ni abiria. Dereva wa Bajaj alikimbia baada ya ajali.
Kilichigusa hisia za wakazi wengi wa jiji ni kuona Mh. Chenge akiendesha gari ambalo Bima yake imeisha. Akiwa ni mwanasheria aliyefikia kuwa mwanasheria Mkuu wa Serikali, inatisha kuona alikuwa anaendesha gari ambalo Muda wa Bima umeisha. Waliopoteza maisha Mungu aziweke mahali pema peponi. Amin.

Wakati huo huo, Tume imeundwa kuchunguza kifo cha dereva wa taxiva Lazaro Mwapi(23 )aliyepigwa risasi na Polisi maeneo ya Stop Over kiwanjani. Inadaiwa kwamba polisi wa kikosi maalum cha kupambana na uhalifu walimshambulia kwa risasi licha ya kijana huyo kutii amri ya kusimama.
Akisimulia tukio hilo dereva anayejulikana kwa jina la Jacob anasema kwamba, "kulikuwa na tukio la ujambazi maeneo hayo na Lazaro alipata mteja na kumshusha alikokuwa anakwenda, wakati akiwa anarudi askari hao walijitokeza katika vichaka na kumsimamisha. Akasimama na kufunga vioo vya gari kwa hofu ya kwamba labda majambazi wanataka kumnyang'anya gari. Walipomwambia ashushe kioo alikishusha kidogo, na ndipo askari mmoja akavunja kioo na kumfyatulia risasi. Inasikitisha, ni kijana mdogo hapa kijiweni na amepewa hiyo gari hata mwezi haujafika"
Mungu ailaze roho ya marehemu Lazaro mahali pema peoni. Amin(picha kutoka blog ya Mroki Mroki)

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker