Friday, March 6, 2009

UPORAJI DAR MCHANA KWEUPEEEE!!!

Ni siku tatu zilizopita nilitoa "Tahadhari" kufuatia dada mmoja kuporwa katika maeneo ya jangwani. Kilichonishangaza ilikuwa saa 3 asubuhi, watu wengi wanapita na foleni ilikuwa kubwa kuanzia jangwani hadi Fire. Ninachotaka kusema hapa nikwamba, watu walikuwa wengi mno kushuhudia hayo yakitokea! Leo nimeona taarifa hii katika blog ya Michuzi nikaona kwa mssisitizo niilete kama ilivyo ili watu waone kwamba sio hadithi ni kweli(Pia soma taarifa yangu hapo chini baada ya taarifa ya Mdau Octavian).

Habari hiyo inasema hivi;

"Leo asubuhi (akiwa na maana 6/3/09) nikiwa kwenye foleni maeneo ya Jangwani saa 1.20 asubuhi, gari la tatu kutoka gari langu kwa nyuma lilivamiwa na vibaka, wakafungua milango ndani ya kama dk 3 wakapora kila walichoweza kupora. Ilikuwa kwenye foleni, jamaa wana visu, na kila mtu akawa anaangalia kama sinema hivi. HAKUNA MSAADA! Watu kwenye daladala la karibu, wakawa wametulia kimyaaa. Na walio kwenye saloon cars wakawa wanafunga vizuri vioo ili wasiwe next target. Siku zote hizi warning nilikuwa sizipi uzito unaostahili, leo nimekubali.Sizungumzii mtu kupora cheni au simu dirishani. Jamaa wamefungua milango, kunyang'anya kila walichokifikia. Tafadhali sio tu ufunge vioo, lakini hakikisha milango imefungwa(LOCKED) BONG TAMBARAREE! Mdau OCTAVIAN 'OC' "

Hiyo ndio taarifa kamili ya Octavian kama ilivyopatikana katika blog ya Mdau Michuzi. na taarifa yangu ya juzi ni hii;
TAHADHARI!
LILE WIMBI LA VIJANA WANAOVAMIA WATU WAKIWA KATIKA FOLENI ZA MAGARI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KUWATISHIA KWA MAPANGA NA MASHOKA, SASA LIMEANZA KUFANYA UHALIFU HUO MAENEO YA JANGWANI . LEO MAJIRA YA SAA 3 ASUBUHI KATIKA FOLENI YA JANGWANI ALIVAMIWA DADA ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA TU LA EDDA, AKIWA ANAENDESHA GARI AINA YA SUZUKI VITARA.VIJANA HAO WALIDAI KUPEWA PESA, SIMU NA VITU VINGINE VYA THAMANI. HUYO DADA AKIWA NA WENZAKE WAWILI, WALIONYESHA KUPINGA AMRI HIYO NA NDIPO VIJANA KAMA 10 WALITOA MAPANGA NA MASHOKA NA KUWATISHIA. BAADA YA KUONA USALAMA WAO UPO HATARINI, WALIAMUA KWAACHIA HANDBAGS NA HAO VIJANA WAKATOKOMEA POLE POLE BILA HOFU YOYOTE.
USHAURI: FUNGA MADIRISHA YA GARI UNAPOKUWA KATIKA FOLENI, JAPO KATIKA MAENEO MENGINE VIJANA HAO INASEMEKANA HUDURIKI HATA KUVUNJA VIOO VYA GARI ILI KUTIMIZA AZMA YAO.

1 comment:

  1. Mmh! twafaaaaaaaaa! yaani sasa Dar inatisha imekuwa Dafur. Wajua sasa hata kutembea barabarani ni mashaka makubwa either uko kwenye usafiri au kwa miguu mmh! jamani ni sababu ya watu kukosa kazi au?

    ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker