Friday, March 20, 2009

TAHADHARI!!!


Kumeibuka wimbi la watu kufanyiwa vitendo vya kiharamia wanapopanda daladala nyakati za usiku au alfajiri. Leo alfajiri kijana anayejulikana kwa jina la Abdu Rashidi Abdalla(27) amepatwa na mkasa kama huo.
Akisimulia wakati akiwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali (MOI), anasema kwamba alitoka nyumbani kwake Manzese saa 11 asubuhi na kupanda daladala kuelekea Kituo cha Mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo. Amesema daladala hiyo ilikuwa na abiria watano na yeye alikuwa wa sita. Daladala lilipokaribia stendi ya mkoa, mmoja wa abiria alianza kumzonga kwamba amemuibia simu yake, wakati wanabishana mara abiria aliowakuta katika gari wakaanza kumpiga. alipofika stendi ya Mkoa na kutoa taarifa kwamba amefika, hawakumsikiliza na gari ikaenda mwendo kasi hadi Kimara ambapo walimtupa nje ya gari huku gari likitokomea kwa mwendo wa kasi.
Anasema, wamempora shilingi laki 2 ambazo alikuwa anampelekea baba yake ambaye ni mgonjwa na mizigo na zawadi alizokuwa anapeleka kwa wazee.
Afisa Uhusiano wa MOI amesema kwamba ni kweli Abdu amepokelewa hapo akiwa ameumia kichwa, sehemu ya bega na michuko sehemu mbalimbali za mwili na anaendelea na tiba.
TAHADHARI: Iwapo ni lazima kupanda daladala nyakati za usiku chukua tahadhari kwa kuandika namba ya usajili ya gari au ya usajili wa daladala inayoonekana ubavuni mwa gari. na iwapo ni gari ambayo haina namba ya ubavuni ya usajili wa daladala, ni vema kuwa na tahadhari. nyingi ya gari zinazofanya uhalifu huu ni zile zinazoitwa 'gari za usiku' yaani 'daladala bubu'.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker