Monday, March 9, 2009

LEO KUTOKA TAASISI YA TIBA YA MAGONJWA YA MIFUPA NA AJALI MUHIMBILI(MOI)


Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ajali Muhimbili (MOI) wameendelea kupokea majeruhi wa ajali kutoka sehemu mbali za jiji na mikoa ya jirani. Taarifa ya Afisa Uhusiano wa MOI Bw. Jumaa Almasi inasema kwamba, wamepokea wagonjwa wafuatao; Simon Nyagogo(36) ambaye ameteguka vifupa vya shingo baada ya ajali.Godfrey Ndunguru(18) kutoka Mwananyamala ambaye amegongwa na gari na kuvunjika mguu sehemu ya paja.Mwingine ni Mohamed Omari Issa(21) aliyevunjika mguu na sehemu ya paja na tayari amefanyiwa upasuaji. Abdul Hamisi(20) ameumia kichwa, na Charles Peter Mkwawa(21) ambaye amevunjika mfupa wa paja. Saidi Hamisi Faundu(25) amevunjika kivundo cha mguu(ankle joint). Mwisho kutoka Dar es salaam ni Nelson Luwangili(35) ambaye amevunjika mguu chini ya goti.

Kutoka Bagamoyo mkoani pwani ni; Manase Kipingu(mtu mzima) ambaye aamegongwa na gari na kupata maumivu ya kichwa(head injury) na Shabani Sanze ambaye aligongwa na pikipiki.

HOJA: Inaonekana MOI inapokea wagonjwa wa ajali kila siku, je askari wa usalama barabarani wanafuatilia hilo na kufanya tathmini ya ajali jijini Dar es salaam?

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker