Monday, March 16, 2009

Leo Kutoka Taasisi Ya Tiba Ya Mifupa na Magonjwa Ya Ajali Muhimbili(MOI)

Pikipiki nazo.....haya!!!

Utafiti uliuofanywa mwisho wa wiki Katika Taasisi ya Mifupa(MOI) unaonyesha kwamba Idadi ya waendesha pikipiki wanaopata ajali bado imesimama juu! kwa mfano katika siku ya jumamosi walikutwa waendesha pikipiki wawili wamelazwa katika Taasisi hiyo wakiwa na majeraha mbalimbali kama ifuatavyo;Godfrey Ndunguru(19) Kutoka Tegeta, amekutwa wodini akiwa amevunjika mguu na kupata majeraha sehemu mbalimbali za mwili. Akielezea tukio hilo anasema kwamba, siku ya tukio yeye alikuwa anaendesha pikipiki za "boda boda" au kwa jina jingine "mchubuko" ambazo hubeba abiria. Alipokuwa njiani abiria wake aliomba asimame ili ajisaidie. Aliegesha pikipiki kando ya barabara akiwa pembeni ya gari. Anasema mara ilikuja gari aina ya toyota 'Chaser' ambayo dreva alionekana kushindwa kuimudu ndipo aligonga pikipiki na kumpitia na yeye!


Mwingine ni Kulwa Slim(37) Mkazi wa Tegeta, Ansema siku ya tukio aligongwa na gari akiwa kwenye pikipiki anatoka Tegeta kwenda Kawe ndipo gari ndogo aina ya Toyota 'Corolla' ilimgonga. Amevunjika mguu wa kulia na kupasuka goti.


Christian Malenda(40) kutoka Morogoro, amevunjika mguu mara mbili . Anasema siku ya tukio alikuwa 'round about' anasubiri gari jingine lipite mara trekta lilikosa mwelekeo na kumgonga.
POLE:Tunawapa pole majeruhi wote na kutoa wito kwamba, ni lazima suala la ajali za pikipiki liangaliwe kwa makini.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker