Tuesday, March 10, 2009

ATHARI ZA KUTOFUNGA MKANDA-WHIPLASH INJURY!







Ni hatari kutofunga mkanda unapokuwa katika chombo cha usafiri. Picha inayoonekana juu ni abiria ambaye hajafunga mkanda na amepitiwa na usingizi. Gari ikifunga breki ghafla anaweza kupiga kichwa mbele au mbele na nyuma na kupata kitu kinachoitwa kitaalam "Whiplash" injury. inatokea kwa muda wa sekunde tu mtu unapiga kichwa mbele katika dashboard ya gari au nyuma ya kiti kama katika mabasi yetu ya abiria na kuvunja vifupa vya pingili za shingo au mgongo. Picha kulia zinaonyesha jinsi whiplash injury inavyotokea na majeraha anayoweza kupata mtu.
Juzi nilitoa habari ya kijana Faki Makame(23) aliyepata ajali na kuvunja vifupa vya pingili za shingo na mgongo na hatimaye kupooza kuanzia shingo hadi miguu. inawezekana kabisa alipata whiplash injury(whiplash injury pictrures from the internet).
DOKEZO: Tafadhali funga mkanda unapokuwa katika chombo cha usafiri kuepusha madhara.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker