Sunday, March 8, 2009

Haya Malori Vipi?
Malori yanalalamikiwa kuwa chanzo kikubwa cha ajali za mara kwa mara katika barabara zetu kubwa. Je, unafikiri lori linapojaza mzigo kama inavyoonekana pichani, na dereva kushindwa kuona nyuma, si ndio mwanzo wa kusababisha ajali?Cha kushangaza ni kwamba, kila kukicha yanapita katika barabara zote. Je wahusika hawayaoni?Au wameridhishwa na hilo? Au kama kawaida ya watanzania, yakishatokea maafa ndio wafungue macho na kuanza kuchukua hatua?

1 comment:

  1. Wazee wa FEVA wakishikishwa kitu kidogo wanayafumbia macho malori kama hayo maana tayari matumbo yao yameshajazwa na ukizingatia wazee wetu wa FEVA wanalipwa mshahara mdogo sana hiyo ndio itafanya "kitu kidogo" kwao isisitishwe na kwa style hii wale wenye mikono mirefu haijalishi anavunja sheria au la watafumbiwa macho tu

    ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker