Thursday, March 5, 2009

LEO KUTOKA TAASISI YA MAGONJWA YA MIFUPA NA AJALI MUHIMBILI(MOI)


Taarifa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) zinasema kwamba wamepokelewa majeruhi wa ajali kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam na mikoa ya karibu. Kutoka Dar es salaam ni majeruhi anayeitwa Ibrahimu Abdallah(62) amepokelewa kutoka Ubungo akiwa amepata maumivu ya kichwa na kuvimba sana kiasi cha kutotambulika kirahisi.

Wengine waliotoka mikoani ni; Aban Kijuu(28) kutoka Arusha ambaye aliangukiwa na axle ya gari walipokuwa wanaipakia ili kuisafirisha. Mentanga Chuma ametokea Kibaha Mkoa wa Pwani akiwa ameumia kichwa na kupata michubuko sehemu mbalimbali za mwili baada ya kupata ajali. Mwingine kutoka Pwani ni Faki Makame Fakha(23), ambaye amepokelewa kutoka Rufiji Health Center, amegongwa na gari akiwa ni mtembea kwa miguu. Baada ya kugongwa amevunjika vifupa vya shingo na vya mgongo, hali ambayo imepelekea yeye kupooza kuanzia shingoni hadi miguuni.

Kutoka Morogoro ni Azizi Idrisa Kilama(22) kutoka Morogoro ambaye aligongwa na gari akiwa anaendesha pikipiki. Amevunjika mguu sehemu ya Paja.Kulingana na maelezo ya Afisa Uhusiano wa taasisi hiyo Bw. Jumaa Almasi, wagonjwa wote wanaendelea na matibabu lakini hali ya Faki ni tete kutokana na kupooza kuanzia shingoni hadi miguuni.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker