Baada ya kujengwa uzio huu katika maeneo ya manzese, ajali za watu kugongwa zilipungua kwa kiwango kikubwa sana. Kabla ya kujengwa uzio huu, kila siku si chini ya watu wawili waligongwa na magari ama yalikuwa yakienda kasi sana ama watembea kwa miguu walikuwa wanafanya uzembe katika kuvuka.
Ni hali ya kusikitisha kuona kwamba, uzio huu umeanza umeanza kutelekezwa baada ya kugongwa na magari kama inavyoonekana katika picha.
HOJA: Kabla hatujaanza kupokea takwimu za vifo vywa watembea kwa miguu, ni vema wahusika wakarudisha uzio huu, na wasichoke kwa kuwa unagongwa na magari mara kwa mara. Unaokoa maisha ya wengi.
No comments:
Post a Comment