Sunday, March 8, 2009

AJALI!AJALI! Mrs Susan Tsivangirai afa ajalini!










Hii ni habari ya kusikitisha lakini inaongeza takwimu za wanaopoteza maisha kwa ajali kila kukicha. Habari si vibaya ikaingia hapa katika Blog la taarifa za ajali.



Susan Tsvangirai(50), mke wa Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai amefariki baada ya kupata ajali.



Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, ajali ilitokana na gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori ambalo lilikuwa na lebo ya USAID.



Mbali na Mama Suzan Tsvangirai, majeruhi ni; Mh. Tsvangirai mwenyewe, dereva wa gari na msaidizi wa Mh. Tsvangirai, na Mh. Tsvangirai mwenyewe. Marehemu ameacha mume na na watoto sita.Mungu awape nguvu famili ya Tsvangirai katika kipindi hiki kigumu.


Habari kutoka ndani ya chama chake cha MDC zilieleza kwamba, bada ya kutoka hopitali Mh. Tsvangirai alipanda ndege na kuelekea Botswana kujipumzisha na atarudi wiki ijayo.


Bw. Tsvangirai alipata mshtuko kumpoteza mkewe wa miaka kwa miaka 31 ambaye wana watoto 6.


Msemaji wa Bw. Tsvangirai, Dennis Murira, anasema kwamba dereva wa lori ameviambia vyombo vya usalama wakati wa mahojiano kwamba, alipitiwa na usingizi wakati anaendesha gari.
Pichani ni Mh. Tsvangirai akiwa na marehemu mkewe Susan, Tsvangirai akiwa na bandeji baada ya kuumia katika ajali na lori lililosababisha ajali.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

1 comment:

  1. Wajua watu hawako serious, inakuwaje msafara wa Waziri Mkuu usiwe na ulinzi? Kuna njia nyingi sana za kupunguza ajali barabarani. Huyo kama kiongozi mkubwa katika nchi alipaswa kuwa na ulinzi katika msafara wake hayo yote yasingetokea. All in all Tunampa pole nyingi Mheshimiwa wetu kwa kumpoteza mwenza wake

    ReplyDelete

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker