Tuesday, March 3, 2009

Mvuvi Afariki Dunia Ziwa Victoria!

Mvuvi aliyejulikana kwa jina moja la Makoye alifariki dunia wiki iliyopita katika ziwa victoria baada ya mtumbwi waliokuwa wakivulia samaki kugongwa na meli ya abiria ya "Nyehunge".Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza jamal Rwambow aliwaambia waandishi wa habari tukio lilitokea eneo la kisiwa kidogo cha mabibi Wilayani Ukerewe.

Alisema, siku ya tukio mvuvi Makoye, akiwa na mwenzake Tema Masugunwa wakivua samaki katika ziwa Victoria, Meli ya "Nyenhunge" mali ya Said Nyenhunge, ilipita kwenye njia yake na kuvuta nyavu zilizokuwa zimeunganishwa kwenye mtumbwi, ambpo ilisababisha mtumbwi huo wenye namba ya usajili MMW 12332 kuvutwa na kujigonga kwenye meli na kuzama pamoja na wavuvi hao wawili na hatimaye Makoye alipoteza maisha (Na Paulina David, Mwananchi)

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker