Wednesday, February 25, 2009

Maumivu.Pichani ni mwananchi ambaye amelazwa katika wodi ya majeruhi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) akiwa na maumivu makali baada ya kuvunjilka ambao unaonekana umewekewa vyuma au "antenna" kama wengi walivyozoea kuuita, lakini kwa jila kitaalam inaitwa "External Fixator" ambavyo husaidia walioumia katika kuunganisha mifupa.
Ni dhahiri kwamba uzalishajii kwa mwananchi huyu umesimama wakati akiwa na wodini na hata baada ya kutoka wodini kwani ataendelea kuuguza mkono kwa muda kidogo.
Tujiulize, anapokuwa wodini au hata baada ya kutoka wodini lakini akiwa katika hali kama hiyo,anazalisha nini, familia yake inapataje mahitaji muhimu? Ni dhahiri kwamba, yeye na familia yeke wanateseka. Swali linakuja, je dereva aliyesababisha haya kwa uzembe anafanywa nini? analipa faini ndogo na baada ya wiki moja anarudi barabarani anafanya uzembe mwingine na kuharibu maisha ya watu wengine?Nafikiri imefika wakati wa kutoa adhabu kali ambazo zitamfanya dereva awe mwangalifu na kufikiria adha atakayopata au kifungo iwapo atashindwa kulipa faini.Nina imani faini kubwa itapunguza kwa kiasi kikubwa uzembe wa madereva. (Picha na Hamisi Bilali)

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker