Madhara ya ajali ni makubwa sana, watu hupoteza viungo na hatimaye kuwa na ulemavu wa kudumu. Kwa miaka mingi nimeshuhudia watu wakiumia kama inavyoonekana pichani na kupoteza viungo kama mikono yote au miguu yote. Hali hii humfanya aliyeumia kuanza maisha mapya ya mahangaiko na taabu kwa sababu anakuwa hawezi kujihudumia kama ilivyokuwa hapo mwanzo alipokuwa na viungo vyote.
Hali hii haimuathiri muumiaji tu, bali husababisha maisha magumu kwa familia na wale wote wanaomtegemea.
Takwimu za SUMATRA zinaonyesha kwamba, asilimia 55 ya ajali husababishwa na uzembe wa madereva. Na mfano mzuri ni wa ajali ya hivi karibuni ambapo dereva wa lori kutokana na uzembe, aligongana uso kwa uso na basi liitwalo Hekima.
Je, wadau tunakubali kuishia katika ulemavu wa kutisha na mateso kwetu na familia zetu? Je, tumekubali kuishia kuwa na ulemavu wa kudumu kwa ajili tu dereva ameamua kufanya mzaha akiwa barabarani? Nafikiri kila mmoja atasema "Hapana". Kama sote tunapingana na uzembe huo, nafikiri ni muda muafaka wa kusema, "NO!" Jamani, tuamke na tuanze kupambana na madereva wazembe hasa hawa wa nabasi ya abiria (picha kwa hisani ya mtandao).
No comments:
Post a Comment