Lori la la kubeba taka liliigonga Bajaj na kusababisha kifo cha mama na mtoto wake. Ajali hiyo ilitokea barabara ya Kawawa eneo la Magomeni ambapo lori hilo kabla ya kuanguka liligonga malori mengine. mashuhuda wanasema kwamba ajali hiyo ilisababishwa na kukatika breki kwa lori hilo. Dereva wa lori alitimua mbio baada ya ajali (Habari hii inapatikana pia katika gazeti la Majira la leo). Lori la kubeba takataka linaloonekana pichani kulia, lina mapungufu mengi lakini bado lipo barabarani na hakuna anayeonekana kushtuka hadi yatokee madhara kama yaliyotokea katika ajali ya leo.
Kwa muda mrefu kumekuwa na kilio cha wananchi kuhusu haya malori ya taka, kama sio yote ailimia kubwa ni mchakavu na mabovu ambapo kuyaona yakipita mbele ya askari wa usalama barabarani bila hata kuulizwa ni kitendawili kisichokuwa na jibu. Nafikiri ni lazima wito wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda uzingatiwe maana kumekuwa na ajali nyingi kutokana na uzembe, iwapo sheria zingezingatiwa maisha ya watu na mali vingeokolewa.
No comments:
Post a Comment