Tuesday, May 19, 2009

Abiria 500 Wakwama Baada ya Behewa Kuanguka Moro!

Abiria takriban 500 waliokuwa wakitoka Dar es salaam kwa treni kuelekea Mkoani Kigoma jana walikwama kwa saa kadhaa katika stesheni ya Mororgoro baada ya treni ya mizigo kuanguka katika stesheni ya Godegode iliyopo katikati ya Kilosa na Dodoma.
Mkuu wa stesheni ya Morogoro, Flavian Nyawale alisema abiria walikwama katika kituo hicho, jana kuanzia saa 5.35 usiku baada ya treni hiyo ya Mizigo kuanguka saa 11.00 jioni Mei 17, mwaka huu na behewa moja kuziba njia wakati ikitokea jijini Dar es salaam.
Nyawale alisema abiria walitarajiwa kuondoka jana saa 1.00 usiku baada ya kukamilika kwa matengenezo ya njia katika eneo ambako ajali ya treni ya mizigo ilianguka.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker