Friday, May 15, 2009

Mtaalam wa 'Nusu-Kaputi' Muhimbili Agongwa na Kufa!

Bakari Atilio mkazi wa Mabibo na mfanyakazi wa kitengo cha nusu kaputi cha hospitali ya Taifa Muhimbili, amefariki baada ya kugongwa na gari. Mkasa wenyewe ulikuwa kama hivi:

Mashuhuda wamesema kwamba Bakari alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 438 ARN maeneo ya mabibo aligongwa na gari ndogo 'taxi' kwa nyuma. aliamua kushuka katika gari lake ili kuangalia uharibifu uliotokana na kugongwa. Mashuhuda wanasema, dereva wa taxi hiyo alirudi nyuma na kukanyaga mafuta hivyo alimgonga na kumburuza hadi chini ya gari.
Kufuatana na ajali hiyo, alivunjika mguu wa kulia(ankle joint), mfupa mkubwa wa paja(femur),mfupa wa shingo(cervical),mbavu na majeraha ya ndani ya mwili(visceral injury).Pamoja na jitihada kubwa za madaktari wa MOI, Bakari alipoteza maisha.Pichani Bw. Bakari akipatiwa matibabu ya dharura.
Ni kitendo cha kusikitisha sana na cha kikatili kilichafanywa na dereva huyo. Tunamwomba Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker