Tuesday, May 5, 2009

MATATIZO YA KIUFUNDI

Samahani wadau naona mtandao ulikuwa unanipa shida kidogo kwa hiyo kwa siku kama mbili sikuwa hewani, lakini sasa hivi tutaendelea kuonana. Karibuni.

2 comments:

  1. Bwana Tram sasa na wewe unaleta lugha za kisiasa? Acha hizo, unaonekana ni mtu poa sana na huna siasa za hivyo hayo mambo ya siasa waachie wenyewe waliozoea huo mchezo mchafu. Wajua kwa nini nalonga hivyo? Lilivyotokea tukio lililotikisa Tanzania, siku ghala la silaha lilipolipuka na kuleta maafa makubwa na kuwaacha wahanga hawana makazi. Tuliambiwa kuwa kilichosababisha hilo ni MATATIZO YA KIUFUNDI, sasa hatuelewi kuwa hayo matatizo ya kiufundi yametokeaje, kama ni suala la joto Dar ina joto la kufa mtu au hawajui nyuzi joto za kutunzia silaha? kama ndivyo mbona miaka yote hayo mambo ni shwari? au kulikuwa na kubeba silala watu kwenda Dalfur kufanya mambo kama minong'ono inavyosemekana mitaani? kuwa walikuwa wanabadilishana wale wa Dalfur walirudi then kulikuwa na kundi lililotakiwa kwenda huko na ndio walikuwa wanabeba silaha? hatujui inabaki kuwa "MATATIZO YA KIUFUNDI". Kuna tofauti gani basi na ule upasuaji tata uliotokea Muhimbili? Kwa nini madaktari walihukumiwa pamoja na wauguzi waliokuwa zamu siku hiyo na wakubwa wao kuandikwa ovyo kwenye magazeti? Kwani na lile halikuwa tatizo la kiufundi? Tuache hapo Bwana Tram, watanzania tuko njia panda maana Nchi nzima imejaa kambi za jeshi, balaa tupu hakuna pa kukimbilia.

    ReplyDelete
  2. Ndugu anonymous, ahsante sana kwa mchango wako, nafikiri tutajenga kwa maoni kama haya tutajenga na kufika pale tunapohitaji kufika.Asante sana mkuu.

    ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker