Thursday, May 14, 2009

Ubovu wa Barabara Wakwamisha Msafara wa Waziri Mkuu Mara Tatu Rukwa!

MSAFARA wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ulichelewa kwa zaidi ya saa tatu kufika kwenye kijiji cha Muze katika bonde la Rukwa kwa sababu ya kukwama njiani mara tatu kutokana na utelezi.
Tukio lilitokea juzi asubuhi wakati akitoka Sumbawanga mjini kwenda kijijini hapo kukagua Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO) cha Muze na kuzungumza na wananchi akiwa njiani kwenda Mamba, wilayani Mpanda kwa ziara ya siku mbili jimboni kwake.
Katika hali ya kawaida, safari ya kuteremka bonde la Rukwa ingechukua saa moja au pungufu ya hapo. Baadhi ya magari yaliyonasa katika utelezi huo ni gari la RPC, gari la walinzi na la Wasaidizi wa Waziri Mkuu.
Utelezi huo ulitokana na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia jana huku barabara aliyopita ya Ntendo hadi Muze ikiwa imemwagiwa kifusi ambacho kilikuwa kimeanza kusambazwa lakini hakijashindiliwa. Barabara hiyo ina urefu wa kilometa 37, lakini sehemu korofi ilikuwa na umbali wa kilometa 15.
Meneja wa TANROADS wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Joseph Nyamhanga alisema barabara hiyo ilikuwa inafanyiwa ukarabati wa awali, ili iweze kufikia kiwango cha barabara zilizo chini ya mradi wa kuzikarabati barabara ili zipitike muda wote ambao ni wa miaka mitano (Source: Mwananchi).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker