Ni madereva wangapi ambao wanajua umuhimu wa taa za nyuma za gari? Mara nyingi nimekuwa nikifuatilia magari mbalimbali yanapita katika barabara za jiji la Dar es salaam na matokeo ni kama inavyoonekana katika picha, magari mengine hayana kabisa hizo taa. Je,wakifunga breki ghafla na kugongwa nyuma watamlaumu nani?Inafurahisha kama unaendesha ukiifuata gari ambayo taa zake zinawaka zote na zina mwanga mzuri-'Bright lights'- kama baadhi ya picha zinavyoonyesha hapa.
Mr. Bobos Class, ni blog inayotoa taarifa mbalimbali za ajali na athari zake.Itangalia ajali zote lakini zaidi zile za barabarani.Mbali ya kutoa taarifa pia inatoa elimu jinsi ya kuzuia ajali na ushauri nasaha kwa waathirika,na jinsi wanavyoweza kupata msaada baada ya kupata athari.Pia Blog hii itaungana na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya ajali kwa njia moja au nyingine, kuelimisha na kutoa ushauri.Blog inatumia Kiswahili na Kiingereza.
Thursday, May 7, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
No comments:
Post a Comment