Tuesday, May 12, 2009

Anateseka baada ya Kugongwa na Pantoni!
Pili Saidi, 46, mkazi wa Kigamboni, akisimulia mkasa uliompata wa kugongwa na pantoni ya ya Mv magogoni mwaka jana, akiwa kama abiria na ilipokosa mwelekeo na kuanza kuyumba, alisukumwa na wakati akianguka ikamgonga.Anasema kuna mtu alipoteza maisha katika tukio hilo.


Ajali hiyo, ilipelekea yeye kuvunjika mguu wa kushoto, kung'oka baadhi ya meno, kuteguka mkono na kuteguka kiuno. Pili, anasema kwamba amekuwa akihangaika kimaisha kwa kuwa tangu aumie katika ajali hiyo amekuwa ni mtu wa kuhangaika kwani hawezi tena kufanya kitu chochote cha kujipatia riziki. "Nimekuwa mtu wa kuhangaika sana ndio maana nilienda ofisi ya Waziri Mkuu ili nipatiwe msaada wa matibabu. Unavyoniona hapa nimetoka ofisi ya Waziri Mkuu kuchukua barua ya kupatiwa matibabu bure MOI".


Huyu mama anasikitisha sana, kwani anayemhudumia ni bibi mtu mzima anayeonekana kuwa na umri wa kama miaka 80 au zaidi(ametokea kidogo pichani).


Ninachojiuliza mimi, kwanini Bima isichukue jukumu la kumpatia msaada huyu mama kulingana na malipo anayotarajia kupata kama hicho kivuko kina Bima? Na je, kama hakina Bima, nani anastahili kulipa fidia ya kuumia kwa huyu mama? Wadau karibuni kwa michango ili tumsaidie Mama Pili Saidi.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker