Friday, May 1, 2009

Leo ni Sikuku ya Wafanyakazi Duniani (May Day)

Leo ni siku ya wafanyakazi Duniani, MAY DAY kama wengi wanavyoifahamu. Wakati watanzania wakisherehekea Sikukuu hiyo wito wangu ni ule ule kwamba, tujihadhari na ajali ili tusiwe sehemu ya takwimu zinazoingia MOI na hospitali nyimgine kila kukicha.


Leo pitapita yangu nilifika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali(MOI) nikapata takwimu za ajali zinaoingia hapo.


Kwa Mujibu wa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Taasisi hiyo, Jumaa Almasi, ni kwamba kuanzia tarehe 26 April mpaka leo hii wamepokea jumla ya wagonjwa 67 kwa mchanganuo ufuatao:
  • 30 wa mabomu kutoka Mbagala,

  • 2 madereva

  • 14 abiria

  • 16 wapita njia

  • 3 waendesha baiskeli

  • 1 amejeruhiwa na mashine

  • 1 amejeruhiwa na treni.
Amesema, Zaidi ya nusu ya wagonjwa hao wamelazwa hospitali wodini. Aliongeza kwamba, wakati mwingine ikitokea ajali kubwa,wanapotea mpaka majeruhi 30 au zaidi! Je, ungependa kuwa sehemu ya takwimu hizi? Tafadhali endesha kwa uangalifu.

Muhimbili Orthopaedic Institute(MOI)

Please, Drive Carefully And don't Be Part Of These Shocking Statistics!

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker