Monday, May 25, 2009

MAONI...!Pamoja na Pole Kwa Mwakyembe.........

Yafuatayo ni maoni ya msomaji wa gazeti la 'Mwananchi' aliyejitambulisha kwa jina moja la Philip kutoka Canada mwenye email; pujap2001@yahoo.com

Nampa pole nyingi Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe kwa ajali aliyopata.Lakini nafikiri halikuwa jambo la busara kwa dereva wake kujaribu kulipita lori lililosababisha ajali hiyo hasa baada ya kuomba njia mara tatu bila mafanikio.
Hiyo ilikuwa ni ishara tosha kwamba dereva wa lori hakutaka apitwe na kwamba angeweza kufanya lolote lile. Kama dereva aliye mbele yako anakataa kukupisha ina maana kwamba huna nafasi kupita.Hata kama alikuwa anataka kuwapisha, kwa kuwa yeye alikuwa mbele, huenda aliona kwamba hapo haikuwa mahali penye usalama kuwaruhusu wapite. Kwa hiyo, walipaswa kuwa wavumilivu.Kama dereva hazingatii kanuni za barabarani, basi ingekuwa jambo jema kuchukua namba ya usajili baada ya kuona kwamba alikuwa hataki kuwapisha yaani kabla ya kujaribu kulipita.Tatu, kwenye mlima na mterenko si busara kupita magari yaliyo mbele yako mpaka unapokuwa na uhakika ni salama kufanya hivyo. Nne, kama ni kweli Dk. Mwakyembe alimwambia dereva wake alipite lori hilo,basi dereva wake angemshauri kwamba si salama kufanya hivyo kwa nguvu.Dereva wa gari anapaswa kuamua mwenyewe bila kufuata ushauri wa abiria.
Wadau mnasemaje juu ya hili?

Shimo lililosababisha ajali ya Dk. Mwakyembe

Gari la Dk. Mwakyembe baada ya ajali.


Picha kutoka: Jamii Forums
No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker