
Mara nyingi nimekutana na waendesha baiskeli wakiwa wamewabeba watoto katika kiti cha nyuma cha baiskeli. Leo asubuhi saa 12.30 nimemuona huyu bwana katika picha(bofya picha) akiwa amembeba mtoto(angalia mshale) ambaye alikuwa anaonekana aidha amechoka au ana usingizi wa kuamshwa asubuhi sana kuwahi shule.Ninachoona mimi, huyu mtoto mikono yake haina nguvu kama ya mtu mzima, njia anayopita ni ina mashimo mashimo na inarusha kiasi kwamba huyu mtoto anaweza kuachia na kudondoka. Naomba tunapoona hilo tukemee ili kunusuru maisha ya watoto kama huyu.
No comments:
Post a Comment