Tuesday, May 19, 2009

Trafiki Hawajasimamia Amri ya Mikanda Katika Mabasi!

Kampeni ya kuweka mikanda na vinakili mwendo katika mabasi yote nchini inaendelea kwa kusuasua na kusababisha kikosi cha Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA), kuongeza muda hadi miezi sita ili wahusika wakamilishe kazi hiyo, baada ya muda wa miezi sita ya awali kutozaa matunda.

Mkuu wa Kikosi hicho, James Komba alisema zoezi hilo halijakamilishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukaidi wa madereva na wamiliki wa mabasi kusembea agizo hilo wakati kazi hiyo haina gharama yoyote.

Kwa ujumla, taarifa hiyo ya kikosi hicho inaonyesha wazi kwamba, kampeni hiyo haina maana ndiyo sababu wameongeza muda bila kuchukua hatua zozote kwa wasiofanya hivyo kama kweli wamedhamiria kupambana na ajali zinazosababishwa na uzembe.

Mpaka sasa watu wengi wanakufa kwa ajali kutokana na uzembe unaosababishwa na madereva kuendesha mwendo wa kasi, pamoja na kutokuwa na vifaa vya kuwasaidia abiria kama vile mikanda katika viti.Hatudhani kuwa vifaa vya kunakili mwendo vinaweza kusaidia kwani, miaka ya nyuma, serikali tena kwa kusimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu waliendesha kampeni ya kuweka vidhibiti mwendo ambavyo havikusaidia.

Kama wamedhamiria kukabiliana na tatizo hilo wanatakiwa kusimamia kikamilifu amri hiyo na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika ndani ya muda uliowekwa, vinginevyo itakuwa sawa na mchezo wa kuigiza ( Source: Mwananchi.co.tz).

Pia Soma http://ajali-traumaclass.blogspot.com/sumatra-na-seat-belts.html


No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker