Saturday, May 9, 2009

School Buses, Mateso au Faraja kwa Watoto?!





Wazazi wengi wanaona kwamba ni bora kumpeleka mtoto katika shule ambayo inatoa usafiri,ili kumpunguzia mtoto adha ya kupambana na makondakta wa daladala na kero nyinginezo zinazoambatana na usafiri huo.
Lakini, sijui kama wazazi wanafuatilia kwa ukaribu kuona kama usafiri huo ni kweli una nafuu kama wao wanavyofikiria au na wenyewe una matatizo makubwa sana. Kwa mfano, wazazi wanajua jinsi magari hayo yanavyojaza? Watoto wanakuwa hawana uangalizi wa kutosha wawapo barabarani?Watoto wadogo kabisa wanapowekwa na wakubwa na kuachwa wasimame kwa umbali mrefu? Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo nawaachia wazazi wayatafakari, wayafanyie uchunguzi.Nimefikia kuandika habari hii baada ya kuona mambo yanayofanywa na watoto waliokuwa katika basi kama inavyoonekana pichani.Walikuwa wanatoa vichwa na mikono nje, kutupa vitu nje bila kujali wapita nje wengine n.k.

No comments:

Post a Comment

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker