Wednesday, May 13, 2009

Ajali Mbaya Kibaha Kwa Matias!


Kuna taarifa kwamba ajali mbaya imetokea maeneo ya Kibaha kwa Mathias, inasemekana watu wawili wamefariki papo hapo na mmoja amefariki akiwa njiani kuelekea taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI).Ajali hiyo imetokea baada lori(fuso) la mchanga kugonga pikipiki na hatimaye kwenda kugonga gari la abiria aina ya 'hiace' lililokuwa na abiria.
Waliofikishwa MOI ni Venosa Liseki(32) ambaye ameumia kichwa na kuvunjika mguu wa kulia na mwingine ni mwanaume ambaye jina halikuweza kupatikana kwa kuwa amepoteza fahamu.
Pichani kulia ni majeruhi Venosa Liseki na kushoto ni majeruhi ambaye hajatambulika.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker