Saturday, May 2, 2009

Kutoka MOI LEO! (A Terrible Daladala Accident!)Sadiki Abdallah mmoja wa majeruhi wa ajali ya leo, ameumia kichwa

Huyu alipata maumivu ya kifua na kuumia ndani kwa ndani......


Huyu aliumia kichwa ,amevunjika mguu na kupasuka mdomo..............Huyu aliumia kiuno, na kuvunjika mguu.....

Huyu binti aliumia kichwa na kupoteza kumbukumbu na kushindwa kutaja jina lake....

Huyu amevunjika mguu............... Huyu kama inavyoonekana pichani amechanika mdomo na kuvunjika mguu pajani

Huyu alipata maumivu makubwa kuliko wote katika ajali hiyo.Ameumia kichwa na kuvunjika miguu yote miwili chini ya goti na mguu wa kushoto ulivunjika sehemu ya paja pia.


AJALI MBAYA ASUBUHI YA LEO

Kama inavyoonekana pichani, majeruhi 10 wamepokelewa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali Muhimbili (MOI) baada ya kupata ajali leo asubuhi mikocheni karibu na nyumbani kwa rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi. Taarifa za kipolisi zimesema kwamba hakuna aliyepoteza maisha.

Baadhi ya majeruhi wamesema kwamba ajali ilitokana na mwendo kasi wa daladala hiyo iliyokuwa inatoka Kariakoo kwenda Kawe.

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano wa MOI, Jumaa Almasi, majeruhi wa2 tu ndio waliruhusiwa kwenda nyumbani. 4 walifanyiwa upasuaji wa dharura, na wa4 walipatiwa tiba na kulazwa kwa uchunguzi zaidi.
Wakati huohuo,Almasi alisema kwamba Majeruhi wa Mabomu yaliyolipuka Mbagala wanaendelea vizuri ispokuwa hali ya majeruhi Zulfa Hamisi ambaye yupo chumba cha wagonjwa mahututi, hali yake bado ni mbaya sana. Na aliongeza kwamba, Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Mh. Shamsi Vuai Nahodha aliwatembelea majeruhi hospitalini hapo.
Mbali na hilo, Bwana Almasi alisema kwamba, tokea jana mchana mpaka leo asubuhi, walipokea majeruhi wa ajali mbalimbali wapatao 18 wakiwemo hao wa ajali ya mikocheni.

Je, watanzania tunaziona hizi takwimu? Je, mdau hapo ulipo umefanya nini kuhakikisha hili janga linatokomezwa?Jana nilisema MOI ilipokea majeruhi wa ajali tu 67, na kuanzia jana mchana hadi leo ni 18 kwa hiyo ndani ya siku7 (April 26 hadi Mei 2) ni wagonjwa 85.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker