
Kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Magonjwa ya Ajali (MOI) kuna taarifa kwamba jioni wamempokea mgonjwa aliyegongwa na pikipiki anayeitwa Sinzia Kiwale(24) ambaye amevunjika mguu chini ya goti. Mbali na hiyo, Afisa Uhusiano wa MOI, Bwana Jumaa Almasi, amesema kwamba usiku wa kuamkia leo walipokea majeruhi wa ajali zaidi ya 20 na 6 wamelazwa katika wodi tofauti za Taasisi hiyo. Waliolazwa ni;Jonas Ndomba(38) mkazi wa pugu ambaye amepata ajali na kuvunjika mkono wa kulia. Mwingine ni mtoto Sadiq Mwala(4) kutoka Mbagala ambaye aliumia kichwa(severe head injury), na Marando 'unknown'(adult) ambaye pia alipata maumivu ya kichwa(severe head injury) kiasi cha kupoteza kumbukumbu na kushindwa kutaja jina la pili. Msafiri Salum(35) kutoka Mtoni alivunjika mguu, Stella Amos(25) kutoka Temeke naye aliumia kichwa(Mild head injury). Na wa mwisho ni Yohana Lohemeja Kutoka Kigamboni ambaye alivunjika mkono.
No comments:
Post a Comment