Thursday, April 16, 2009

Ajali ya Jahazi, 20 Wahofiwa Kufa Maji!

Habari kutoka jiji la Tanga zinasema kwamba, Jahazi ambayo ilikuwa inaelekea Pemba kutoka Tanga ilipata ajali ya kuwaka moto hivyo ili kunusuru roho zao abiria waliamua kujirusha majini, na wengine walijirusha baada ya kuungua sehemu mbalimbali za mwili.
Habari za kipolisi zinasema kwamba, jahazi hiyo ilikuwa na mizigo na abiria wapatao 40.Abiria wapatao 20 wameokolewa na 20 hawajajulikana wako wapi.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga Simon Sirro, amesema kwamba wanajaribu kufuatilia kwanini jahazi hiyo ilikuwa na kibali cha kuondoka saa 11jioni lakini ikaondoka yapata saa3.30 usiku.
Baadhi ya abiria walionusurika wansema kwamba, ilifika saa 7 usiku wakiwa katikati ya bahari, mara wakaona moto unatokea upande wa injini.
Siku chache zilizopita SUMTRA walitoa agizo la kuzuia vyombo vidogo kutembea wakati wa usiku ili kuzuia ajali kama hizi. Pia Soma hii; (http://ajali-traumaclass.blogspot.com/2009/03/sumatra-yazuia-vyombo-vidogo-vya-majini.html).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker