Sunday, April 5, 2009

MOI Yateuliwa Kuwa Kituo Kikuu cha Upasuaji!

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili(MOI)-Muhimbili Orthopaedic Institute- imeteuliwa kuwa kituo kikuu cha upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu nchini, kufuatia kuwasili kwa madaktari bingwa watatu wa upasuaji toka nje.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Blandina Nyoni,alisema Tanzania ni kati ya nchi ambazo bado hazijawa na madaktari bingwa katika nyanja ya upasuaji wa ubongo(Neurosurgery).
Alisema kwamba kwa miaka kadhaa nchi ilikuwa na madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo wapatao watatuai na , ambao wanatakiwa kutoa huduma kwa watanzania wote wenye matatizo kama hayo nchi nzima.
Alisema kuwasili kwa madaktari hao bingwa kutoka Marekani ili kusaidia wale waliopo hapa nchini kutasaidia kuwapo uwiano wa datrari na wagonjwa anaowahudumia katika fani hiyo. Alisema hali hiyo italeta uwiano wa daktari mmoja kwa wagonjwa milioni 1 kuliko ilivyo sasa ambapo daktari mmoja kwa wagonjwa 21.7.
Aliongeza kwamba asilimia 98 ya wagonjwa waoumia vichwa na wengine kuhitaji upasuaji wa ubongo hupoteza maisha kutokana na ukosefu wa wataalam wa fani hiyo(Neurosurgery).
Madaktari hao kutoka marekani watakaa nchini kwa miaka mitano wakitoa mafunzo kwa madaktari wa hospitali zote hapa nchini.
yES! HII NI HABARI NJEMA KWA WATANZANIA KWANI NCHI NZIMA IMEKUWA IKITEGEMEA WATAALAM WA UPASUAJI WA UBONGO WATATU(3)AMBAO WOTE WANAPATIKANA MOI. JAMBO AMBALO KWA HAKIKA LIMECHANGIA KWA KIWANGO KIKUBWA UPOTEVU WA MAISHA YA WAGONJWA WAPATAO AJALI(TRAUMA) NA AMBAO WALIKUWA WANAHITAJI HUDUMA YA MADAKTARI HAO.KWANI MTU AMBAYE AMEPATA AJLI AKIWA KIGOMA, MWANZA, LINDI NK NA HAIWEZEKANI YEYE KUSAFIRISHWA KUJA DAR ES SALAAM(MOI) KWA HAKIKA ATAPOTEZA MAISHA! INAFAA KUTOA PONGEZI KWA MAMLAKA HUSIKA KUANZISHA PROGRA KAMA HIYO IKIWA NA LENGO LA KUONGEZA UFANISI NA IDADI YA WATAALAM KATIKA FANI HIYO.
MOI, Muhimbili Orthopaedic Institute has been appointed as the 'Center of Excellence in Neurosurgery' whereas other institutions in Tanzania will send their doctors for training at MOI.Thanks to the efforts by the Ministry of Health and Social Welfare, to bring in 3 doctors from America who could work with MOI Neurosurgeons in training doctors and treatment of various patients in need of spine and brain surgery.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker