Wednesday, April 8, 2009

Huu ni Uzembe Wa Hali ya Juu!


Jana nilishuhudia uzembe huu katika barabara ya Morogoro eneo la Mbezi. Dereva wa basi amesimama mahali ambapo si kituo ,kiasi kwamba lori lililokuwa linakuja nyuma ya basi lilionekana kabisa kwamba breki zake si nzuri na dreva alianza kubabaika. Waliokuwa wanashusha mizigo kutoka katika basi (angalia picha) hawakuonekana kujali hatari iliyokuwa inawakabili. Sisi tuliokuwa tunakuja kutoka upande mwingine tulianza kuchanganyikiwa baada ya kuona dereva wa lori ameanza 'kupanic'.Angalia gari nyeupe (baloon).

nafikiri askari wa usalama barabarani wawe wana-patrol na madereva kama hawa watozwe faini kubwa sana, naamini watajirekebisha.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker