Saturday, April 18, 2009

Je Askari "wanaotanua" Wanalinda Sheria za Barabarani?

Nimekutana na habari hii katika website ya 'JAmii Forums', nafikiri ni vema nikiiweka hapa pia ili wadau wengi zaidi waione na kutoa michango yao. Najua inawagusa wengi!!!
"Mara nyingi nimekuwa nikiona kwenye 'traffic jam' madreva wa magari ya jeshi la polisi au JWTZ wakiwasha 'emergency lights' na kutanua na halafu wakishapita magari mengine yanawafuata nyuma na kusababisha msongamano mkubwa sana kwa vile madreva wa magari hayo huwa nao wanapata mwanya wa kutanua. Cha ajabu ni kwamba mara zote hukuti gari la askari yeyote likishikiliwa na 'taffic police' kwa kuvunja sheria za barabarani.
Hivi hapa huwa ujumbe wake ni upi: kwamba askari hawezi kuvunja sheria isipokuwa raia tu au nini?Siku moja nilikuta polisi mmoja kwa sababu ya kutanua kwake na madreva wengine kumfuata akiwa amesababisha 'traffic jam' kubwa sana na akawa yeye mwenyewe anaanza kufokea watanuaji wenzake kwa kuziba njia. Niliona ni ujinga mkubwa wa kujifanya kwa vile yeye ni askari basi anakuwa juu ya sheria. Kwa kweli nilimpuuza sana na nikaona askari wa aina yake hawastahili kuwa katika jeshi hilo. Naomba tuchangie kwa hili na wahusika wapelekewe taarifa hizi. Binafsi huwa inanikera sana nikiona haya!
Pili hili la bajaji; kweli ni sahihi kwa kauli niliyosikia? Mimi naona madreva wa daladala hasa zile zinazomillikiwa na wakubwa ndizo zina madreva na makondakta vichwa maji kwa vile wanajua hata wakivunja sheria hakuna kitakachofanyika dhidi yao.Naona kudhani kwamba madreva wa bajaji ndio wanaosababisha ajali barabarani ni kukwepa kutatua tatizo la ajali barabarani. Pengine ni mradi wa wakubwa au pengine wamilki wa bajaji wengi si vigogo: mbona kungekuwa na mikakati kama hiyo ambayo imetangazwa kuhusu babajai ajali za magari zingepungua? Naona hapa tunachezewa akili na wakubwa.Mara nyingi nimekuwa nikiona kwenye 'traffic jam' madreva wa magari ya jeshi la polisi au JWTZ wakiwasha 'emergency lights' na kutanua na halafu wakishapita magari mengine yanawafuata nyuma na kusababisha msongamano mkubwa sana kwa vile madreva wa magari hayo huwa nao wanapata mwanya wa kutanua. Cha ajabu ni kwamba mara zote hukuti gari la askari yeyote likishikiliwa na 'taffic police' kwa kuvunja sheria za barabarani. Hivi hapa huwa ujumbe wake ni upi: kwamba askari hawezi kuvunja sheria isipokuwa raia tu au nini?Siku moja nilikuta polisi mmoja kwa sababu ya kutanua kwake na madreva wengine kumfuata akiwa amesababisha 'traffic jam' kubwa sana na akawa yeye mwenyewe anaanza kufokea watanuaji wenzake kwa kuziba njia. Niliona ni ujinga mkubwa wa kujifanya kwa vile yeye ni askari basi anakuwa juu ya sheria. Kwa kweli nilimpuuza sana na nikaona askari wa aina yake hawastahili kuwa katika jeshi hilo. Naomba tuchangie kwa hili na wahusika wapelekewe taarifa hizi. Binafsi huwa inanikera sana nikiona haya!Pili hili la bajaji; kweli ni sahihi kwa kauli niliyosikia? Mimi naona madreva wa daladala hasa zile zinazomillikiwa na wakubwa ndizo zina madreva na makondakta vichwa maji kwa vile wanajua hata wakivunja sheria hakuna kitakachofanyika dhidi yao.Naona kudhani kwamba madreva wa bajaji ndio wanaosababisha ajali barabarani ni kukweta kutatua tatizo la ajali barabarani. Pengine ni mradi wa wakubwa au pengine wamilki wa bajaji wengi si vigogo: mbona kungekuwa na mikakati kama hiyo ambayo imetangazwa kuhusu babajai ajali za magari zingepungua? Naona hapa tunachezewa akili na wakubwa(imeandikwa na T. Magobe).

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker