Wednesday, April 15, 2009

Uzembe kusambaratisha ndoto za Charles?(Shattered Dreams?)


Kijana Mathias Charles mwenye umri wa miaka 22(pichani) ambaye anaishi Machimbo, Kitunda, amepata kilema cha kudumu kwa kupoteza mkono wa kulia kutokana na ajali iliyosababishwa na uzembe, japo aliyefanya uzembe huo sasa hivi ni marehemu kwani alifariki kutokana na ajali hiyohiyo. Akielezea mkasa uliompata, kijana Charles anasema "Nilikuwa naendesha baiskeli nikiwa na mzigo wa sausaages ambazo namuuzia bosi wangu, nilifika maeneo ya Gongo la Mboto mlima wa Magereza, ghafla nikaona pikipiki inakuja kwa kasi sana, nilipokuwa najaribu kufikiria jinsi ya kuikwepa niliona imeniganga na kuniburuza hatimaye nikapoteza fahamu. Sikujua kilichotokea nikashtuka nikiwa hospitalini nimejaa damu huku kichwa na mkono vinaniuma sana. Muda huo fahamu zilirudi na nikagundua kwamba mkono wangu hautamaniki,uliharibika sana.Madaktari walijaribu sana kuuokoa lakini ikashindikana hivyo ukakatwa".

Dereva wa pikipiki ambaye alisababisha ajali hiyo, alikutwa amelewa lakini alipoteza maisha.

Kijana Charles anasema kwamba, alitoka Magu kijiji cha Guliati kuja Dar es salaam kutafuta maisha, lakini sasa amepata kilema anahofia kwamba labda ndoto zake hazitatimia.

yES! Nampa pole kijana Charles, na kwamba kupoteza kiungo sio mwisho wa maisha, bado ana nafasi ya kufanikisha ndoto zake.
No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker