Ni hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) ilitoa tamko la kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha kwamba vyombo vyao vinakuwa na mikanda ya abiria(seat belts),lakini kinachoonekana ni kwamba wananchi pia hawajapata elimu ya kutosha juu ya matumizi na umuhimu wa mikanda hiyo. Hivi karibuni nilisafiri kwa basi la kampuni ya Scandinavia lenye namba za usajili T540 AGE,ambalo tayari lina mikanda hiyo lakini hakuna hata abiria mmoja aliyekuwa amefunga mkanda.Inaonekana dhahiri kwamba abiria waliokuwamo katika basi hilo hawajui hata matumizi ya mikanda hiyo.Nafikiri kinachotakiwa kwanza ni kuwatayarisha wananchi wafahamu umuhimu na kuwakumbusha mara kwa mara. Nchini Kenya wao walianzisha kampeni kama hiyo na wananchi walikuwa nafunga mikanda pale tu ilipotangazwa kwamba abiria atakayekiuka agizo hilo atatozwa faini na mwenye basi kufungiwa leseni ndipo waliona umuhimu wa kufunga mikanda na kikosi cha usalama barabarani kilikuwa kinasimamamisha magari na kukagua ili kuona ni nani hajafunga mkanda.Nafikiri kinachotakiwa kutangulia ni uhamasishaji na elimu ya kutosha ndipo adhabu kwa kukiuka agizo zianze kuetekelezwa.
Wananchi wanatakiwa kutambua ni kwanini wanahimizwa kufunga mikanda, na nina imani kwamba wakitambua hilo, hakutakuwa na haja ya kutumia nguvu ya ziada.Pia soma habari hii; http://ajali-traumaclass.blogspot.com/2009/03/mikanda-ni-muhimu-kwenye-mabasi.html
Abiria wakiwa wametulia raha mustarehe bila kufunga mikanda.Mshale katika picha unaonyesha kifungio (buckle) cha mkanda kikining'inia chini bila kufungwa.
Abiria akiwa hana wasiwasi, mkanda unaning'inia pembeni kama mshale unavyoonyesha.
No comments:
Post a Comment