Saturday, April 4, 2009

Inatatiza Sana!!

Kuna kitu kimoja ambacho kinanitatiza sana kutokana na ongezeko la ajali hapa nchini. Iwe ni ajali za majini au nchi kavu, zote hizi zimeongezeka kwa kiwango cha kutisha. Lakini natatizika kwa sababu, hapo zamani za kale kwa mfano safari za majini hazikuwa na maendeleo ya kiteknolojia kama yaliyopo sasa.
Meli za wakati huo zilitegemea usomaji wa nyota na kuendeshwa kwa nguvu ya upepo(angalia picha za merikebu za zamani). Sasa hivi meli zina kila kitu,kuanzia matumizi ya injini na radar ambazo huweza kusoma mwendo wa meli au mahali iendapo kwa ufasaha zaidi kuliko ilivyokuwa miaka hiyo. Si hivyo tu, hata usomaji na utabiri wa hali ya hewa nao umefikia kiwango cha juu kiasi cha kujua ni mwelekeo gani kuna dhoruba na inakwenda kwa mwendo kasi kiasi gani.
Hayo yote ni maendeleo ambayo kila mtu aanategemea kwamba yatapunguza ajali za vyombo vya majini kwa kiwango kikubwa. Lakini hivyo ndivyo sivyo. Ajali zinaongezeka kila kukicha.
Kwa upande wa vyombo vya nchi kavu hali ni mbaya zaidi. Ajali zimekuwa nyingi kwa kiwango cha kutisha. Kulingana na maelezo ya Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI), ongezeko la ajali limepelekea wodi kujaa sana kutokana na kwamba kiwango cha ajali ni kikubwa kuliko idadi ya vitanda vya wagonjwa katika taasisi hiyo.
Natatizika kwamba teknolojia kweli inatusaidia au nayo inachangia katika wimbi hili la ongezeko la ajali?
(Paintings from http://tripas-art-gallery.blogspot.com; Photo by Silvan Kivyale).

2 comments:

 1. Thank you for your comments on my work/blog. Salute you on your job which is one of most difficult.
  Will be following you :))

  best
  -nivi

  ReplyDelete
 2. Thanx nivi, am a great fan of your work. Let us keep in touch, for sure i know we have to learn from each other.
  Tram Almasi

  ReplyDelete

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker