Wednesday, April 15, 2009

Ujumbe Kwa TANROADS!

Picha zinazoonekana sio kwamba zina kiwango duni, la hasha! zilipigwa alfajiri ya leo (saa 11.40) maeneo ya njia ya Msewe kupitia chuo Kikuu cha Dar es salaam eneo la Mlimani.
Labda nianze kwa kusema kwamba, Barabara ya Morogoro imekuwa na "kero" kubwa ya msongamano wa magari, iwe ni asubuhi au jioni.Kwa ajili hiyo, madereva wengi wanajaribu kutafuta njia ambazo zitawakimbiza kutoka katika foleni na hii imepelekea kutumia njia za pembezoni kama hiyo ya kutokea Bahama Mama(Kimara Baruti) hadi Chuo Kikuu kwa kupitia Msewe.
Maoni yangu ni kwamba, kama barabara hii itatengenezwa ni hakika magari mengi yatatumia barabara hiyo na hivyo kupunguza msongamano Barabara ya Morogoro. Kama ilivyotengeneza njia ya 'mkato' kutoka Kawawa Road hadi kwa Sheikh Yahya nafikiri ni jambo la busara kwa TANROADS kutengeneza njia hiyo ya Msewe na ile ya kutoka Jangwani kupitia Kigogo hadi 'Ubungo Maziwa' kwa kiasi kikubwa itapunguza msongamano wa magari.


Huu ni msongamano wa magari leo asubuhi wakijaribu kupita njia fupi ya Msewe kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa lengo la kukwepa foleni.


4 comments:

  1. Umenena Mr. Bobos Class!Nimewahi kukaa Ubungo Msewe kwa miaka takribani minne na kishuhudia jinsi njia hii ilivyo busy kwa magari kila asubuhi na jioni.Ina umuhimu mkubwa kama ulivyobainisha, nakumbuka kero zilizokuwa zikitupata kipindi cha mvua, utelezi na magari kukwama, yote hayo ikiwa ni pilika za kukwepa foleni ya Morogoro Road!TANROAD waamke!

    ReplyDelete
  2. Mwanasosholojia, natumai tukiungana na kuwaamsha TANROADS labda watafanya linalotakiwa kufanywa ili kukabiliana na hali hii. Unajua tunapoteza muda mwingi wa kuzalisha kwa ajili ya kukaa kwenye foleni.Kila kukicha kero ya foleni inaongezeka. si njia tatu wala nini, ambayo ilitatua tatizo hili.Kama bajeti ya kuweka fly-overs haipo(kitu ambacho nina uhakika)basi hizi 'feeder roads' zifanyiwe kazi.

    ReplyDelete
  3. Nimekusoma mkuu, umeamsha hisia zangu, muda si mrefu tunawagongea hodi tena TANROADS, mpaka kieleweke

    ReplyDelete
  4. Haswaa,kwa nguvu zote lazima kieleweke.

    ReplyDelete

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker