Friday, April 3, 2009

Kutoka MOI Leo!


Kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali Muhimbili(MOI) ni taarifa ya kusikitisha ya kijana Athumani Steven Mwakipesile(28) ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo kufuatia ajali aliyopata baada ya kusukumwa na kondakta wa daladala inayofanya safari zake kati ya Mbezi na kariakoo. Kulingana na maelezo ya kijana huyo, ni kwamba alitoa noti ya Sh. 10,000 ili konda akate Sh. 250 ya nauli yake. Alipofika Magomeni na kuomba chenji,'konda' alikataa kumpa na kumsukuma nje ya gari ndipo akadondoka chini ya gari na tairi za gari hiyo zikamptia sehemu za kifuani na kumkanyaga mguu wa kushoto.

Hivyo athumani amevunjika mbavu na mguu (fracture of left femur) na kupata maumivu yaliyopelekea afanyiwe upasuaji wa dharura .

Anachoweza kukumbuka ni kwamba gari ilikuwa DCM yenye namba T 738....hakuweza kukumbuka namba zote, lakini anasema taarifa zipo polisi na wanaendelea kuitafuta hiyo gari.

Yes!imekuwa ni kitu cha kawaida kwa makondakta kuwanyanyasa abiria, ni lazima SUMATRA na vyombo vingine vifanye kazi ya ziada kudhibiti hali hii. Kijana Athumani angeweza kupoteza maisha kirahisi tu!

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker