Sunday, April 26, 2009

Hatari Kwa Kijana Huyu!

Kijana unayemuona nyuma ya lori linaloonekana pichani, ni mlemavu ambaye amepoteza miguu yote, haijulikani ni kwa ajali au kwanini.Amejifunza kutembea kwa kutumia magoti, kwani inaonekana miguu ilikatwa chini kidogo ya goti. Mara nyingi anapatikana maeneo ya taa za kuongozea magari za Magomeni aidha kwa upande wa Barabara ya Kawawa au Morogoro.Anachofanya hapo huomba msaada wa pesa katika magari yanayopita njia hizo.
Ninachotaka kuongelea hapa ni hatari ya kijana huyo kugongwa na gari kwani wakati mwingine hukaa katikati ya barabara.
 Si magari yote yana breki nzuri au hata kama gari lina breki nzuri, zinaweza kuleta matatizo na hivyo kupelekea yeye kugongwa.
Leo Dar es salaam kulikuwa na mvua kubwa, nimemkuta maeneo hayo hayo. Kipindi cha mvua magari mengi huwa na matatizo ya breki,na pia magari huserereka yanapofunga breki.Je hiyo si hatari kwake? Je,askari wa usalama barabarani hawana jukumu la kumuelimisha huyu kijana?Mara nyingi anakuwa karibu na askari muongoza magari iwe asubuhi au jioni au hawamuoni? siamini hivyo!
Kuna haja ya kumuepusha huyu kijana na hatari hii, kwani naona hatari inayomkabili mbeleni.

No comments:

Post a Comment

This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker