Wednesday, April 8, 2009

Mwathirika Ajali ya Treni 2002 Bado Anasota(June 2002 Train Accident Victim!)


Mzee Raphael Tondo(65) pichani, ni mmoja kati ya watu waliopata ajali iliyotokea Igandu karibu na Dodoma mwezi June 2002, ambapo treni ilipata matatizo ya breki. Watu 281 inaaminika walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa akiwamo mzee Tondo.
Leo hii nilikutana na mzee huyo akiwa anapata matibabu Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ajali(MOI), na anasema kwamba leo ni siku yake ya kuja kufanya 'check-up' kwani toka aumie katika ajali amekuwa ni mtu wa maumivu muda wote. "Huu ni mwaka wa 7 toka ajali ile, lakini mpaka kufikia leo bado ninaumwa, na bado sijapata malipo yangu ya Bima ambayo yangenisaidia mimi na familia yangu kwani toka wakati huo sijaweza tena kufanya kazi".
Mzee Tondo alipata maumivu ya kichwa(severe head injury) na ikafikia kipindi alikuwa anaanguka kama kifafa. Anashukuru sana MOI kwani alikuwa anapata matibabu kwa msamaha(exemption). Jambo ambalo anasema kama si hivyo sijui hali yake ingekuwaje.
yES! Ninachojiuliza mimi ni kwamba, inakuwaje huyu mzee anahangaikia malipo ya Bima kwa miaka 7 sasa. Nafikiri kuna mahali tatizo lipo. Tunajaribu kuwasiliana na kampuni inaitwa Legal Assistance for Accident victims ili kuangalia ni kwa jinsi gani mzee Tondo anaweza kupata msaada.

1 comment:

  1. Me nimoja wa watu nilikuepo katika ajali Ila Leo kwenye hii habar tareh aijaandikwa

    ReplyDelete

blogarama - the blog directory
Directory of News Blogs
This blog gives information about accidents-vehicles,motorcycles,bycycles etc,also highlights the suffering of those involved in various accidents. It gives counselling to the accidents victims and information as to where they can get assistance be it legal or humanitarian.
Health blogs
eXTReMe Tracker